Mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo amesema anaimani chini ya kocha mpya wa klabu hiyo Eric Ten Hag watashinda makombe na amemtakia kila la kheri. CR7 pia amethibitisha anafuraha kuwepo klabu hapo.
Akifanya mahojiano na Televisheni ya Manchester United Ronaldo amemtakia kila la kheri kocha mpya wa kikosi hicho Mholanzi Ten Hag katika maandalizi kuelekea msimu ujao wa mashindano.
''Najua alifanya kazi nzuri akiwa Ajax na ni kocha mwenye uzoefu. Lakini tunahitaji kumpa muda na mambo yanahitaji kubadilika jinsi anavyotaka. Natumai tutakuwa na mafanikio bila shaka. Kwa sababu ikiwa utafanikiwa, Manchester yote itafanikiwa pia. Kwa hiyo namtakia kila la kheri. Tumefurahi na kufurahishwa, sio tu wachezaji lakini mashabiki pia. Namtakia kila la kheri na tuwe na matumaini kwamba mwaka ujao tutashinda vikombe.'' Amesema Ronaldo
Msimu uliopita 2021-22 Ronaldo alimaliza akiwa mfungaji bora wa Manchester United akiwa na mabao 24 kwenye michuano yote katika michezo 35. Mchezaji huyo mara 5 wa Dunia mkataba wake na The Red Devil unamalizika Juni 2023 na ameweka wazi kuwa anafuraha kuwa ndani ya kikosi hicho.