Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo ana njaa kama kijana wa miaka 18

Ronaldo (19).jpeg Ronaldo ana njaa kama kijana wa miaka 18

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unaambiwa kocha wa timu ya taifa ya Ureno Roberto Martínez anadai kuwa hakuna mtu mwenye njaa kali ya kufunga mabao kama Cristiano Ronaldo.

"Cristiano Ronaldo ana njaa kama vile mchezaji wa miaka 18. Yeye ni mfano wa kuigwa. Kila mara anajaribu kuwa katika nafasi sahihi na anatafuta nafasi za kufunga magoli," amesema Roberto Martínez.

Timu ya taifa ya Ureno mpaka hivi sasa katika michezo 10 waliyocheza ya kuwania kufuzu michuano ya EURO 2024 wamefanikiwa kushinda yote huku Cristiano akiongoza kwa wafungaji akiwa na jumla ya mabao (10).

Je, ni nyota gani mwingine unadhani ana njaa ya kufunga kama Ronaldo?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live