Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo amtaka Luis Enrique United

Luisenriquecropped Blt1trcihanl1srqorra0644s Luis Enrique

Mon, 22 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati dunia ikiamini kuwa Manchester United inafanya mipango ya kumpa ajira Zinedine Zidane kuwa kocha wa timu hiyo, inadaiwa staa wa timu, Cristiano Ronaldo anapendekeza jina la kocha mwingine kabisa.

Ronaldo anataka Luis Enrique ndiye awe mrithi wa Solskjaer badala ya Zidane ambaye wamewahi kufanya kazi pamoja na kwa mafanikio makubwa Real Madrid.

Makocha wengine wanaotajwa kuwa wanaweza kupata nafasi ya kuinoa Man United ni Erik ten Hag wa Ajax, Mauricio Pochettino wa Paris Saint-Germain na Brendan Rodgers wa Leicester City.

Enrique amekuwa akiinoa Hispania tangu mwaka 2019, kocha huyo mwenye umri wa miaka 51 aliifundisha Barcelona kwa mafanikio makubwa akibeba La Liga mara mbili na Champions League mara moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live