Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo amshawishi Messi akacheze Saudi Arabia

Messi X Ronaldo UEFA.jpeg Ronaldo amshawishi Messi akacheze Saudi Arabia

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imefichuka! Lionel Messi amefunguka alikuwa anatamani sana akacheze ligi moja na hasimu wake, Cristiano Ronaldo kabla ya kujiunga na Inter Miami ya Marekani.

Messi amekiri alishawishika kumfuata Cristiano Ronaldo akacheze kwenye Saudi pro League na angecheza dhiodi ya hasimu wake huyo na anaamini ushindani wao ungekuwa mkubwa.

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia amekuwa na athari kubwa katika soka Marekani, baada ya kuisaidia Inter Miami kubeba Kombe la Ligi kwa mara ya kwanza akicheza pamoja na wachezaji wenzake wa zamani wa Barcelona Jordi Alba na Sergio Busquets.

Licha ya kujiunga na Inter Miami, Messi amefichua alikuwa na chaguo la kuhamia kwenye ligi ya Saudi Pro akachuane na mpinzani wake Ronaldo.

Messi aliiambia Time: “Chaguo langu la kwanza lilikuwa ni kurejea Barcelona, ​​lakini haikuwezekana. Nilijaribu kurudi, lakini haikutokea. Pia ni kweli baadaye nilikuwa nafikiria sana kwenda Saudia, Naifahamu Saudi Arabia ina ushindani mkubwa kwenye soka. Katika mawazo yangu ilikuwa Saudi Arabia au Marekani kwani ligi zote zilinivutia sana.”

Saudi Pro League imewekeza fedha nyingi kuleta wachezaji mwenye majina makubwa kama Ronaldo, Neymar na Karim Benzema, lakini imeshindwa kumpata Messi licha ya ofa nono kutolewa.

Messi alichagua kwenda Marekani na athari yake ilionekana na imeripotiwa tayari imeuza tiketi za msimu wa 2024, licha ya tiketi kupanda bei baada ya Messi kutua.

Kuwepo kwa staa huyo wa kimataifa Argentina, watu maarufu walishawishika kwenda uwanjani kwa ajili yake kama LeBron James, Camilla Cabello, DJ Khaled, Kim Kardashian na mastaa wengine wakali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live