Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo ampongeza Clara Luvanga kwa kutwaa Ubingwa Saudia

Ronldo X Clara Luvanga Ronaldo ampongeza Clara Luvanga kwa kutwaa Ubingwa Saudia

Sun, 17 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Al Nassr ya wanawake anayocheza nyota wa Tanzania Clara Luvanga imetwaa ubingwa wa ligi kuu wanawake nchini Saudi Arabia mara baada kushinda mchezo wao dhidi ya Al Hilal kwa goli 4-2 huku Clara akitupia moja nyavuni.

Hadi sasa Al Nassr wamecheza michezo 11 na kufikisha alama 31 huku wakibakiza michezo mitatu tu kukamilisha ratiba ya ligi kwani katika michezo hiyo Al Nassr wamezoa alama 31 huku timu inayowafuatia ikiwa na alama 18 na kushindwa kuwafikia kwa idadi ya michezo iliyobaki.

Clara Luvanga anaongoza mbio za ufungaji bora akilingana mabao na mshambuliaji Ibtissam wote wakiwa na magoli 10 huku Clara akimzidi mshindani wake kwa usaidizi wa mabao akiwa na asisti 3 hadi sasa Ibtissam hana asisti hata moja.

Kupitia mtandao wa instagram wa nyota wa Al Nassr Cristiano Ronaldo amewapongeza timu hiyo ya wanawake kupitia insta story yake.

Hilo linakuwa taji la kwanza kwa Clara Luvanga kwenye ligi alizowahi kucheza kwenye maisha yake ya soka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live