Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo ampiku Harry Kane

Ronaldo 40 Cristiano Ronaldo

Thu, 28 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Al-Nassr amempindua Harry Kane na kufikisha mabao 53 kwenye kalenda ya mwaka 2023, baada ya kufunga mabao mabao mawili katika ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya timu ya Karim Benzema, Al-Ittihad katika mchezo wa Ligi Kuu Saudi Arabia.

Kwenye orodha Kane alikuwa anaongoza akiwa na mabao 52 baada ya kucheka na nyavu dhidi ya Wolfsburg kwenye mechi ya Bundesliga wiki mbili zilizopita akifuatiwa Ronaldo nafasi ya pili.

Straika huyo wa Bayern Munich alipania kumaliza mwaka 2023 akiwa kinara wa mabao katika orodha ya wafungaji bora duniani ili awakimbize Ronaldo na Erling Haaland anayekipiga Manchester City.

Kwa mujibu wa Kane aliamini kwamba Ronaldo hatacheka na nyavu kabla ya sikikuu ya Krismasi ili asimpite hata hivyo mambo yamekuwa tofauti.

Aidha kutokana na Bundesliga kusimama kwa ajili ya mpumziko ya mwisho mwaka, huenda Ronaldo akaongeza idadi ya mabao wikiendi hii.

Hiyo inamaanisha kwamba Ronaldo ndiye anaongoza katika orodha ya wafungaji bora duniani akifuatiwa na Kane, Kylian Mbappe na Haaland.

Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha TNT Sports, nyota wa Paris Saint-Germain, Mbappe na Haaland wamefunga mabao 50 kila mmoja.

Straika wa Roma, Romelu LUkaku na nyota wa Fluminense, German Cano mwenye umri wa miaka 35 kwa pamoja wamcheka na nyavu mara 39.

Kutokana na mabao mawili aliyofunga Ronaldo, staa huyo wa kimataifa wa Ureno amefikisha mabao 19 kwenye Ligi ya Saudi akiwa ndiye kinara wa mabao katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu. Jumla ana mabao 21 katika mashindano yote aliyocheza msimu huu akiwa na uzi wa All-Nassr.

Staa huyo wa zamani wa Real Madrid na Manchester United atakuwa na matumaini ya kumaliza mwaka 2023 kwa kucheka na nyavu dhidi ya Al-Taawoun kwenye mechi nyingine ya Ligi Kuu Saudi Arabia utakaochezwa kesho kutwa.

Kutokana na ushindi wa Al-Nassr imeendelea kujikita nafasi ya pili ikiwa na pointi 43 ikizidiwa pointi saba na Al-Hilal kwenye msimamo wa Ligi ya Saudi baada ya kucheza mechi 18.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live