Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo ampiga bao Messi mtandaoni

Messi X Ronaldo Saudia Ronaldo ampiga bao Messi mtandaoni

Wed, 20 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Cristiano Ronaldo ameendelea kuwakimbiza mastaa wenzake kwenye mitandao ya kijamii na amekuwa ndiye binadamu anayefuatiliwa kwa muda wote katika historia ya soka akiwamo mpinzani wake, Lionel Messi.

Kwa mujibu wa mtandao wa Google, nyota wa klabu ya Inter Miami na timu ya Taifa ya Argentina, Messi hamfikii Ronaldo na ikifuchuliwa staa huyo wa kimataifa wa Ureno anawavutia zaidi mashabiki duniani kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii zaidi ya mchezaji yoyote ikiwamo Instagram ambako ndiye mwanamichezo anayefuatiliwa zaidi akiwa na mashabiki zaidi ya 600 milioni.

Inaelezwa kila anachofanya Ronaldo inakuwa ni stori kubwa mtandaoni, tofauti na Messi licha ya kufanya mambo makubwa kwenye soka na mambo mengine nje ya uwanja na Ronaldo ni moja ya majina yanayoongozwa kwa kutafutwa kwenye mtandao wa Google.

Ronaldo ameshinda tuzo tano za Ballon d’Or, huku akitengeneza historia katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Staa huyo amebeba mataji mengine ya ligi alipokuwa anakipiga Manchester United, Real Madrid na Juventus na kunyakua ubingwa wa Euro akiwa na kikosi ch Ureno mwaka 2016 na yote hayo yalimwongezea umaarufu wa kuzidi kufuatiliwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kwa mujibu wa Google.

Kwa sasa ana umri wa miaka 38, ameendelea kuwa mfungaji bora wa muda wote katika mashindano ya Ulaya na mechi za kimataifa na katika timu yake mpya ya Al Nassr inayoshiriki Ligi Kuu ya Saudi Arabia na kuipa pia umaarufu timu hiyo kutokana na kufuatiliwa kwake tangu alipojiunga nao akitokea Man United.

Ronaldo ameweka rekodi ya kufunga mabao mengi mwaka 2023, akiwa tayari ameshaweka kambani mabao 50, pia ameisaidia Ureno kufuzu michuano ya Euro itakayofanyika Ujerumani mwakani.

Chanzo: Mwanaspoti