Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo ampa mtoto wa Piers Morgan viatu alivyofungia bao la Europa

Ronaldo Spencer Morgan.jpeg Ronaldo ampa mtoto wa Piers Morgan viatu alivyofungia bao la Europa

Thu, 17 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Machester United Cristiano Ronaldo amempa mtoto wa Mtangazaji maaruufu kutoka Uingereza, Piers Morgan viatu ambavyo alivivaa wakati akifunga bao lake katika Ligi ya Uropa mnamo Oktoba 27 dhidi ya Sheriff.

Ronaldo ametanda kwenye vichwa vya habari baada ya mahojiano aliyoyafanya na Morgan kuanza kusikika.

Katika mahojiano hayo nyota huyo aliwalaumu waajiri wake na wachezaji wenzie wengine wa zamani kwa mambo kadhaa akiwemo Erik ten Hag, Ralf Rangnick na Wayne Rooney.

Kupitia mtandao wa Instagram, Spencer Morgan (29) ameposti picha akiwa ameshikilia viatu hivyo na vilevile aliposti video inayomuonyesha Ronaldo akithibitisha kuwa viatu vile ni vya kwake.

Picha hiyo iliambatana na ujumbe huu “Krismas imekuja mapema sana mwaka huu.

Asante sana Cristiano kwa viatu ulivyovitumia ulipopiga goli lako la mwisho la Manchester United. Sasa wacha tukutafutie klabu mpya.”????

#KitengeSports

Chanzo: www.tanzaniaweb.live