Cristiano Ronaldo alionekana kama kumkataa kijanja mchezaji mwenzake wa zamani Gary Neville kabla ya mechi ya Ligi Kuu ya Manchester United dhidi ya West Ham Jumapili mchana.
Ronaldo aliamua kumpuuza Neville baada ya mchambuzi huyo kumkosoa kwa kushindwa kuonesha kiwango bora wakati wa ushindi wa United dhidi ya Tottenham.
Neville alisema United watakuwa ‘bora zaidi bila’ Cristiano na kwamba wababe hao wa Premier League wanapaswa ‘kumaliza uhusiano wao’ na mchezaji huyo.
Ronaldo hakufurahishwa na maoni ya Neville na alidhirisha hisia zake kabla ya pambano la United siku ya Jumapili.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 alienda kuonana na mchezaji mwenzake wa zamani Louis Saha, ambaye alikuwa akifanya kazi kwenye jopo la wachambuzi wa Sky Sports. Uamuzi wa Cristiano kumkataa Neville ulikuja baada ya mchambuzi huyo kumkosoa na kueleza tabia yake kuwa ‘haikubaliki’.
Gary Neville getting aired by Cristiano Ronaldo... ???????? pic.twitter.com/UpKAmNjw1v
— Sky Sports Premier League (@SkySportsPL) October 30, 2022
Akizungumza kabla ya pambano la United na Chelsea wiki iliyopita, Neville alisema: ‘Imekuwa wiki kubwa kwa Erik ten Hag, uchunguzi wote juu yake na uhusiano wake na Ronaldo.
“Lakini lazima niseme sidhani kama aliachwa na chaguo lingine. Hiyo ni mara ya pili kwa Cristiano kuondoka Old Trafford kwenye gari lake kabla ya wachezaji wenzake kuingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo, na niseme kwamba, kwa mtazamo wa chumba cha kubadilishia nguo – ni jambo ambalo halikubaliki.”