Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo amaliza ukame Man United ikikwea nafasi ya nne

Cristiano Ronaldo Manchester United 14sbiw66jkezw1sph4rduh1dz9 Magoli ya Ronaldo na Bruno yaipa ushindi United mbele ya Brighton

Wed, 16 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kukosa ushindi katika mechi tatu za mwisho kwenye Ligi mechi mbili na moja Kombe la FA, Manchester United imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Brighton katika mchezo wa Ligi Kuu England mtanange uliopigwa dimba la Old Trafford Leo Jumanne.

Ushindi huo unaifanya Manchester United inayofundishwa na kocha wa muda Ralf Rangnick kukwea mpaka nafasi ya nne kwa muda kabla ya timu nyingine kucheza.

Katika mchezo huo, staa Cristiano Ronaldo amefunga goli nzuri akimaliza ukame wa mechi sita bila kufunga ambapo bao la pili limefungwa na Bruno Fernandes ambaye alitumia vyema pasi ya Paul Pogba.

Mechi hiyo pia imeshuhudiwa, mlinzi wa Brighton Lewis Dunk kutolewa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu kufuatia kumnyima nafasi ya goli winga wa Man United Anthony Elanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live