Fri, 6 Jan 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Kwa mujibu wa sheria za Saudi Arabia ni kuwa huwezi kuishi na Mwanamke nyumba moja kama hamjafunga ndoa kwa kuwa taifa hilo linafuata sheria za kiislamu na hivyo inambana moja kwa moja Ronaldo na Mchumba wake Georgina.
Lakini kwa mujibu wa jarida la EFE ni kuwa Ronaldo hatoguswa na sheria hiyo kwakuwa wanamtazama kama ‘Mfanyakazi’ aliyekuja kuitangaza nchi yao, lakini bado Wahafidhina wanasisitiza Ronaldo amuoe Mpenzi wake ili maisha yaendelee.
Ronaldo kwa sasa maisha yake ni nchini Saudi Arabia ambako anakipiga katika klabu yake mpya ya Al-Nassr
Chanzo: www.tanzaniaweb.live