Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo aiweka sokoni ndege yake

SPORT PREVIEW RONALDO PLANE Cristiano Ronaldo

Wed, 6 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkongwe wa Manchester United Cristiano Ronaldo (37) ameiweka ndege yake sokoni kwa kuwa imekuwa ndogo mno kwake.

Ndege hiyo aliyoinunua mwaka 2015 ina thamani ya takribani dola za kimarekani milioni 25.

Hali kadhalika, inayo spidi ya 560mph, ina uwezo wa kuchukua watu 7 hadi 10, ina mitambo ya intaneti, jokofu, tanuri n.k na mara kwa mara hukodishwa pale ambapo nyota huyo anakuwa haihitaji.

Mshambuliaji huyo mahiri huitumia ndege hiyo aina ya Gulfstream G200 kwa safari za mapumziko pamoja na familia yake, safari za kwenda kwao Portugal na safari zingine nyingi ndani ya bara la Ulaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live