Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo ainusuru Man U na kichapo Ulaya

Skysports Cristiano Ronaldo 5569583 Cristiano Ronaldo, alifunga mabao mawili jana katika sare ya magoli 2-2 vs Atalanta

Wed, 3 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bao la dakika ya mwisho la Cristiano Ronaldo usiku wa jana, limeisaidia Manchester United kupata sare ya magoli 2-2, na wenyeji Atalanta katika mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Gewiss mjini Bergamo.

Josip Illicic alianza kuifungia Atalanta dakika ya 12, kabla ya Cristiano Ronaldo kuisawazishia United dakika ya 45+ baada ya kupigiana pasi safi na Bruno Fernandes.

Duvan Zapata akawafungia la pili wenyeji, Atalanta dakika ya 56, kabla ya Ronaldo kuisawazishia tena United dakika ya 90.

Kwa sare hiyo, United inafikisha pointi saba na kuendelea kuongoza Kundi F kwa wastani wa mabao tu dhidi ya Villarreal, wakati Atalanta imefikisha pointi tano na Young Boys yenye pointi tatu inashika mkia baada ya wote kucheza mechi nne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live