Alhamisi usiku timu ya taifa ya Ureno ilicheza mechi yake ya kwanza katika mashindano ya kombe la duni ya mwaka huu nchini Qatar dhidi ya Nyota Weusi, timu ya taifa ya Ghana.
Mechi ambayo iliweka historia katika mashindano hayo kwani Ghaja japo walilemewa kwa mabao matatu kwa mawili, walikuwa timu ya kwanza kabisa kutoka Afrika kufunga bao katika mashindano hayo nchini Qatar.
Katika mechi hiyo ambayo ilikumbwa na utata mwingi kutoka kwa refa hasa baada ya kuwatunuku Ureno penalty yenye utata iliyotiwa wavuni na staa Ronaldo, mchezaji huyo alionekana akifanya kitendo ambacho kimeibua gumzo kali mitandaoni.
Katika video moja ambayo imekuwa ikisambazwa mitandaoni, Ronaldo alionekana akitoa kitu fulani ndani ya kaptula yake upande wa mbele katika sehemu yake nyeti na kukitia mdomoni kabla ya kuanza kukitafuta huku akikimbia.
Kitendo hicho kimeibua mjadala mkali huku kila mtu akionekana kuachwa kinywa wazi kwani mpaka sasa hakuna anayejua Ronaldo ni kitu kipi kile alikitoa katika tupu yake ya mbele na kutia mdomoni, na hata yeye mwenyewe hajazungumzia video hiyo.
Katika mechi hiyo, Ghana walijitahidi kwa udi na ambary kutafuta ushindi huku Ureno nao wakicheza vizuri hadi kipindi cha kwanza kikakamilika bila timu yoyote kuona lango la mwingine.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo Ureno walipata penalty yenye utata baada ya benki kumuangusha Ronaldo aliyeinuka na kutia penalty kinywani. Wachezaji wenza Joao Felix na Rafael Leao walifunga mabao mengine mawili na Ghana kufunga yao mawili kupitia wachezaji Andre Ayew na Osman Bukari ambaye aliiga kusherehekea maarufu kwa Ronaldo.