Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo afutiwa kesi aliyotuhumiwa kubaka

Ronaldo Kesi Ronaldo afutiwa kesi aliyotuhumiwa kubaka

Sun, 12 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi ya kudaiwa kumbaka Kathryn Mayorga iliyokuwa ikimkabili Cristiano Ronaldo nchini Marekani imefutwa na Jaji Jennifer Dorsey aliyekuwa akiiendesha.

Kathryn alidai nyota huyo wa Manchester United alifanya tukio hilo walipokuwa hotelini Las Vegas, Marekani mwaka 2009. Ronaldo alikana na kusema walielewana na hakumbaka, lakini alimlipa mwanamke huyo Dola 375,000 (Tsh. Milioni 871) ili wamalize kesi nje ya Mahakama.

Licha ya kupata fedha hizo, baadaye Kathryn alirejesha kesi na kuanza kumsumbua Ronaldo, mshitaki na wakili wake wakimtishia kwa nyaraka za siri walizokuwa nazo, ambapo Jaji ameona si sahihi na ndipo akaifuta kesi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live