Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo afunga bao la 50 la mwaka katika ushindi wa Al-Nassr

Ronaldo Afunga Bao La 50 La Mwaka Katika Ushindi Wa Al Nassr Ronaldo afunga bao la 50 la mwaka katika ushindi wa Al-Nassr

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Cristiano Ronaldo alifunga bao lake la 50 mwaka huu wakati Al-Nassr ilipowafunga wapinzani wao Al-Shabab 5-2 na kutinga nusu fainali ya Kombe la Mfalme wa Saudia.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid na Manchester United aliifungia timu yake bao la nne katika kipindi cha pili.

Hilo lilimfanya kufikisha mabao 26 msimu huu, huku 16 kati ya mabao hayo akifunga katika mechi 15 za Saudia Pro League.

Siku tatu zilizopita, Ronaldo alicheza mechi ya 1,200 katika taaluma yake katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Al-Riyadh.

Alifunga bao moja na kuchangia kufunga jingine katika mchuano huo

Chanzo: Bbc