Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo afikisha magoli 801, aandika historia katika Soka

Ronaldo Ronaaaldo Cristiano Ronaldo

Fri, 3 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshindi mara tano wa tuzo ya Ballon D'or, Cristiano Ronaldo usiku wa jana aliifungia Manchester United magoli mawili katika ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Arsenal.

Magoli hayo mawili yamempeleka nyota huyo katika rekodi nyingine ambapo amekuwa mchezaji wa kwanza kufikisha magoli 801 katika career yake kwa upande wa klabu na timu ya Taifa.

Ronaldo ndie anaeongoza kwa mchezaji aliefunga magoli mengi kwa timu ya taifa upande wa wanaume, Ligi ya mabingwa na klabu ya Real Madrid.

Ronaldo amefikisha idadi hiyo ya magoli akiwa ameshacheza michezo 1097, huku Sporting CP akiwa aimeifungia magoli 5, Man United magoli 130, Real Madrid magoli 450, Juventus magoli 101 na Timu ya Taifa ya Ureno magoli 115.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live