Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo aendelea kumkalisha Lionel Messi

Messi Si Rafiki Yangu Lakini Namheshimu   Christiano Ronaldo.png Ronaldo aendelea kumkalisha Lionel Messi

Sun, 15 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mujibu wa tovuti ya Forbes, Cristiano Ronaldo ndio mchezajia anayelipwa zaidi duniani kwa mwaka huu ambapo anakunja Pauni 214 milioni.

Ronaldo amekuwa mmoja kati ya wachezaji wanne wa ligi ya Saudi Arabia ambao wamewekwa kwenye orodha ya wachezaji 10 wanaolipwa pesa nyingi zaidi duniani.

Kwa upande wa Ligi Kuu England, Erling Haaland ndio anaongoza akifuatiwa na Mohamed Salah ambaye kama angekamilisha uhamisho wa kutua nchini Saudi Arabia katika dirisha lililopita basi angekuwa anashika nafasi ya pili au ya tatu.

Forbes imemueweka Ronaldo namba moja kwa pesa hiyo kwa sababu anakunja mshahara wa Pauni 164 milioni kwa mwaka lakini anapata pia Pauni 49 milioni kutokana na madili yake nje ya uwanja.

Pesa hizo za ziada ni mjumuisho wa pesa alizopata kupitia matangazo aliyoyafanya ambayo ni kuhusu pambano kati ya Tyson Fury na Francis Ngannou linalotarajiwa kufanyika Riyadh, Saudi Arabia, pia tangazo la kutangazi siku ya kitaifa ya Saudia.

Mastaa wengine wanaocheza Saudia waliotokea kwenye orodha hii ni Neymar, Karim Benzema na Sadio Mane ambao wameshika nafasi ya tatu (Neymar), ya tano (Benzema) na yanane (Mane).

Lionel Messi ameshika nafasi ya pili nyuma ya Ronaldo yeye akiwa anakunja jumla ya Pauni 111 milioni wakati Neymar yeye akipata Pauni 92 milioni na anafuatiwa na staa wa Paris Saint-Germain Kylian Mbappe na Haaland anayeshika nafasi ya sita akiwa anakunja Pauni 48 milioni.

Kwa upande wa pale England Salah yupo nafasi yapili yeye akiwa na uwezo wa kupata Pauni 44 milioni wakati Kevin De Bruyne akiwa nafasi yatatu kwa Pauni 32 milioni ambazo zimechangiwa sana na dili la kuwa balozi wa kampuni ya McDonald ndani ya Ubelgiji.

Mchezaji wa mwisho kati ya hawa 10 ni Harry Kane anayepata Pauni 30 milioni ambazo zimechangiwa kwa kiasi kikubwa na ubalozi wake na kampuni ya Online retail firm Fanatics alilosaini mapema mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live