Cristiano Ronaldo alicheza mechi yake ya kwanza ya katika klabu mpya ya Al Nassr katika ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Ettifaq kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Saudia siku ya Jumapili.
Mshambulizi huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 37 alijiunga na klabu hiyo mwezi uliopita kwa mkataba utakaodumu hadi 2025, akiripotiwa kulipwa zaidi ya £177m kwa mwaka.
Aliongoza safu ya mashambulizi na kucheza mchezo mzima ambao kiungo wa Brazil Talisca alifunga bao la ushindi.
Al Nassr wako kileleni mwa ligi ya Saudia, pointi moja juu ya Al Hilal iliyo nafasi ya pili.
Ronaldo ambaye aliwahi kuzichezea Manchester United, Juventus na Real Madrid - alilakiwa na mabango na shangwe kutoka kwa mashabiki wake wapenzi kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha King Saud mjini Riyadh.
Haya yanajiri baada ya kufunga mabao mawili akiichezea Riyadh All Star XI katika mechi walioshindwa kwa idadi ya magoli 5-4 dhidi ya timu ya Lionel Messi ya Paris St-Germain kwenye mechi ya kirafiki manmo Alhamisi.