Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo aandika rekodi nyingine ya kibabe

We Ronaldo Cristiano Ronaldo

Wed, 21 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Cristiano Ronaldo ametunukiwa Cheti cha Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa kuwa mchezaji wa kandanda wa kiume aliyetokea kwenye mechi nyingi zaidi za kimataifa.

Nahodha wa Ureno Cristiano Ronaldo alifunga bao la ushindi dakika ya mwisho katika usiku wake wa kihistoria akiwa mchezaji wa kwanza kwa wanaume kushinda mechi 200 za kimataifa katika ushindi wao wa kufuzu Euro 2024 dhidi ya Iceland.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 aligeuza mpira wa kichwa wa Goncalo Inacio kutoka karibu na goli.

Bao hilo awali lilikataliwa kwa kuotea kwa Inacio lakini lilikubaliwa baadae na mwamuzi msaidizi kupitia video (picha za marejeo)

Hilo lilikuwa goli la 123 la Ronaldo kwenye kimataifa, akiendeleza rekodi yake ya dunia.

Ronaldo wa Al-Nassr alivunja rekodi ya mshambuliaji wa Kuwait Bader Al-Mutawa ya kucheza mechi 196 mwezi Machi – na alipewa cheti na Guinness World Records kabla ya kuanza kwa mchezo huo kuashiria alama hii ya hivi punde.

“Kwangu mimi ni mafanikio ya kushangaza, ni ya kushangaza,” alisema baada ya mechi. “Na, bila shaka kufunga bao la ushindi, ni muhimu zaidi.

“Hatukucheza vizuri sana lakini wakati mwingine soka huwa hivyo lakini tulifunga bao na, kwa maoni yangu, tulistahili. Nina furaha sana kwa sababu ya mechi 200, lakini hii ni maalum zaidi.”



Ronaldo yuko katika mwaka wake wa 20 kuichezea Ureno, akiwa amecheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa mwaka 2003, na bado ni mchezaji wa kawaida katika timu hiyo licha ya kuondoka Ulaya na kuelekea Saudi Arabia baada ya Kombe la Dunia.

Mshambulizi huyo wa zamani wa Sporting Lisbon, Manchester United, Real Madrid na Juventus ameshinda tuzo ya Ballon d’Or mara tano.

Bao lake la tano la kufuzu kwa Euro 2024 lilisaidia Ureno kushinda mara nne kati ya mechi nne.

Iceland, ambao wameshinda mara moja pekee, Willum Willumsson alitolewa nje kwa kadi nyekundu mara mbili zikiwa zimesalia dakika 10 kumalizika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live