Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo: Ubingwa wa Dunia hautamaliza mjadala wa Messi

CR 7 Mjadala Cristiano Ronaldo

Mon, 21 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Cristiano Ronaldo anatumai kuwa anaweza kuwa mtu wa kumshinda Lionel Messi katika michuano ya Kombe la Dunia 2022, lakini haamini kwamba ushindi wa Kombe la Dunia kwa Ureno utamaliza mjadala wa soka kuhusu Messi.

Ronaldo na Messi ndio magwiji wawili wa kisasa wa mchezo huo, huku wafuasi wa kila mchezaji wakidai kuwa wao ndio bora zaidi wakati wote, Lakini licha ya mafanikio ya Ubingwa kwa Euro na ushindi wa mwaka jana wa Argentina katika Copa America, hakuna kati yao aliyewahi beba Kombe la Dunia.

Ronaldo amevumilia msimu mgumu katika klabu ya Manchester United, lakini amewasili Qatar akiwa na hali ya kujiamini, hata kama haamini kwamba ana lolote la kuthibitisha katika yale yanayoendelea.

Ronaldo amesema kuwa; “Hata kama ningeshinda Kombe la Dunia, kungekuwa na mjadala huu ni kama katika kila kitu, kuna wengine wanapenda kuongea zaidi, wengine kuongea uzushi”

Yeye ni mchezaji mwenye tamaa zaidi na anasema kuwa angependa kushinda kombe hilo, lakini ikiwa hatashinda bado angefurahi kwa kila kitu ambacho amefanya hadi sasa. Kama watu wangemwambia hataweza kushinda taji hilo, angejivunia kwa ambavyo amefanya.

Cristiano anasema kuwa kushinda Kombe la Dunia ilikuwa ni ndoto kwake, na inawezekana lakini wataona anatumaini nguvu zote ziko upande wao. Kama Ureno na Argentina kila moja ikishinda kundi lake, wawili hao hawatakutana uwanjani hadi fainali ya Desemba 18.

“Ilikuwa ni kampeni ambayo nimekuwa nikifanya, ambayo nimekuwa nikiitaka kwa miaka mingi, nimetimiza ndoto ya kuweza kuifanya na itakuwa Kombe langu la tano la Dunia. Nina umakini na nina matumaini makubwa kwamba mambo yatakwenda vizuri”

Mchezaji huyo pia hakusita kuongelea kuhusu yeye na Messi kuonekana wote wamepiga picha wakiwa wanacheza mchezo wa Chess na kusema kuwa; “Checkmate sisi kufanya katika maisha, si tu katika chess. Na mimi kufanya hivyo mara nyingi”

Ronaldo na Messi wamekutana mara mbili pekee katika viwango vya Kimataifa, huku Ureno na Argentina wakishinda mechi moja ya kirafiki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live