Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo, Henderson nusra wazipige kavu kavu

Ronaldo Henderson(15).jpeg Ronaldo, Henderson nusra wazipige kavu kavu

Sat, 4 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Cristiano Ronaldo na Jordan Henderson walihusika katika mzozo kufuatia mchezo mkali wa Kombe la Mfalme kati ya Al-Nassr na Al-Ettifaq.

Picha za muda wote zinaonyesha Ronaldo alijibizana maneno ya hasira na Henderson baada ya Al-Nassr kuibuka na ushindi wa bao 1-0 baada ya bao la Sadio Mane.

Mara kwa mara Ronaldo alimuonyesha ishara kiungo huyo wa kimataifa wa England kabla ya kuingia kwenye mzozo mkali kati yao katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha King Saud mjini Riyadh.

Mjadala kati ya nyota huyo wa zamani wa Manchester United na nahodha wa zamani wa Liverpool uliendelea hadi walipotoka nje ya uwanja, huku Ronaldo akionekana kurusha mikono yake hewani na kutikisa kichwa. Henderson alionekana akijaribu kumtuliza nyota huyo wa Ureno wakati wanaelekea vyumba vyao vya kubadilishia nguo.

Henderson, ambaye aliondoka Liverpool na kujiunga na Al-Ettifaq inayonolewa na Steven Gerrard katika hatua ya kushangaza kipindi cha usajili kiangazi alizua taharuki wakati timu yake ilipochapwa 1-0 huku akiepuka kadi nyekundu licha ya kumsukuma beki wa Al-Nassr, Otavio mara mbili.

Pia, Ronaldo alitaka mwamuzi abadilishwe wakati wa pambano la robo fainali kwani amekasirishwa na uchezeshaji wake dakika za mwisho za kipindi cha kwanza.

Mchezaji mwenzake Anderson Talisca alionekana kuipatia Al-Nassr bao la kuongoza katika dakika za mwisho lakini bao lilikataliwa na mwamuzi baada ya  VAR kudai mfungaji alikuwa ameotea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live