Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo, Arteta wabeba tuzo EPL

Pjimage (35) Washindi wa mwezi Septemba

Fri, 8 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Manchester United, Cristiano Ronaldo ameibuka mchezaji bora wa mwezi Septemba Ligi Kuu Engaland.

Ndani ya mwezi Septemba, Cristano Ronaldo amecheza mechi tatu akiwa na United na kufunga magoli matatu.

Katika kinyang'anyiro hicho Ronaldo amewapiku Joao Cancelo (Man City),Antony Rudiger(Chelsea), Saint-Maximin(New Castle),Mohammed Salah (Liverpool) na Ismail Sarr(Watford).

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta ameibuka Meneja Bora wa mwezi Septemba akiwapiku Guardiola, Klopp, Potter na Smith.

Arsenal imecheza mechi mechi tatu na kushinda zote na ameruhusu goli 1, ndani ya mwezi Septemba.

Goli Bora la mwezi limekwenda kwa winga wa Everton, Andy Townsend na goli lake dhidi ya Burnley huku ikiwa ni mara ya tatu kwa mchezaji huyo kushinda goli bora la mwezi katika maisha yake ya soka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live