Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo 17, Man United 13

RONALDO 7777 Ronaldo 17, Man United 13

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Manchester United ikianza vibaya msimu wa 2023/24 kwa kupoteza mechi tano (5) kati ya 9 kwenye michuano yote mpaka sasa, mshambuliaji wake wa zamani Cristiano Ronaldo ambaye anakipiga Al Nassr FC ya Saudi Arabia ameanza msimu kwa kishindo.

Mpaka sasa msimu huu Cristiano Ronaldo amefunga magoli 17 kwenye mechi 17 kwenye michuano yote akiwa na Al Nassr FC.

Ronaldo aliondoka Manchester United baada ya kuvunja mkataba na klabu hiyo kwa makubaliano ya pande zote na kuondoka klabuni hapo mnamo Novemba 22, 2023 baada ya kutofautiana na Meneja Eric Ten Hag kwa kile kilichodaiwa ni utovu wa nidhamu.

Hata hivyo baada ya kuondoka kwake Manchester United haijapiga hatua kubwa kulingana na Mreno huyo ambaye mpaka sasa msimu huu yeye peke yake amefunga magoli 17 huku klabu nzima ya Manchester United ikifunga magoli 13 tu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live