Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldinho afunga mtaa London

Ronaldinhoooooooooooooooo Ronaldinho afunga mtaa London

Mon, 3 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Supastaa, Ronaldinho amezua balaa zito huko London baada ya kusababisha mashabiki kujaa barabarani kiasi cha kufunga njia na kusababisha foleni kubwa.

Kabla ya mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa juzi Jumamosi huko Wembley, supastaa huyo wa Kibrazili aliwasili England, Ijumaa iliyopita.

Ronaldinho, 44, alipita kwenye mitaa ya London akiwa kwenye gari la Rolls-Royce lenye rangi ya pinki na tiki la Nike ubavuni. Baada ya kushuka kwenye gari, Ronaldinho alikuwa na kibeji chake na viatu vipya vya soka na alipoonekana jambo hilo liliwafanya mashabiki kuanza kujaa eneo hilo.

Mashabiki walianza kujaa na simu zao wakimpiga picha staa huyo. Watu hao waliongezeka na kufanya barabara isipitike na kusababisha msongamano mkubwa wa magari.

Baada ya hapo, mashabiki waliandika kwenye mitandao ya kijamii, ambapo wa kwanza aliandika: “Nimemshuhudia Ronaldinho huko Shepherds Bush. Wala sioni aibu kusema kwamba nilipagawa.”

Mwingine aliongeza: “Nimemwona Ronaldinho na hakika kabisa nimesahau kila kitu.”

Shabiki wa tatu aliandika: “Yeye ni mungu wa mpira.” Na mwingine alisema: “Anatikisa kila mahali anapokwenda.”

Chanzo: Mwanaspoti