Thu, 26 Oct 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mwandishi nguli wa Habari za michezo Fabrizio Romano amethibitisha kuwa Lionel Messi ndiye mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa jarida la habari la Ufaransa la France Football ‘Ballon d'or’
Romano anadai viashiria vyote vipo ukingoni kuthibitishwa lakini Messi ndiye mshindi wa mwisho wa tuzo hiyo itakayotangazwa siku ya Jumatatu Oktoba 30, 2023.
Hii itakuwa tuzo ya 8 kwa Messi tatu zaidi ya mpinzani wake wa muda mrefu Cristiano Ronaldo mwenye ballon d’or 5.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live