Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Roma kumpa Mkataba mpya Mourinho kwa Masharti haya

Jose Mourinho Portugal.jpeg Kocha wa AS Roma Jose Mourinho

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Roma wanaripotiwa kukaribia kwenye makubaliano na Jose Mourinho kuhusu kuongezewa mkataba ambao utamfanya meneja huyo wa Ureno aendelee kusalia katika klabu hiyo.

Katika wiki za hivi karibuni, mengi yamesemwa kuhusu mkataba wa Mourinho na klabu hiyo wakati huu ambapo imesalia miezi michache tu kumalizika kwa mkataba wake.

Inaripoti kuwa Roma wameamua kuendelea kupata huduma ya 'The Special One' kwa angalau kwa mwaka mwingine na wanaharakisha makubaliano yaweze kufikiwa kabla ya mwezi Februari.

Taarifa za kuaminika zinasema mkataba huo huenda ukawa na masharti fulani yanayohusishwa na kufuzu kwa timu kwenye Ligi ya Mabingwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live