Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Roho iliyopaa Mbinguni

Sir Bobby Charton Sir Bobby Charton.

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Roho ilifika kwenye mafupa ya koo,ikafika kwenye ncha za vidole kwa ajili ya kuthibitisha kila kilichotokana na tone la manii lazima kionje ladha ya kifo, hakika katika jambo hili Mwenyezi Mungu hakuwahi kudanganya pale aliposema popote mtakapokuwa yatawafika mauti hata mkiwa kwenye ngome madhubuti.

Basi Mwenyezi Mungu siku ya Oktoba 21, 2023 aliamua kuichukua roho ya Sir Bobby Charton bila kujali umri na umaarufu wake,lengo sio kututoa machozi sisi mashabiki wa Manchester United isipokuwa kutupa taarifa kwamba binadamu ambaye ameishi kwenye tumbo la mwanamke ndani ya miezi 9 kaburi litakuwa ndio nyumba yake ambayo atalala usingizi wa milele akiwa ndani ya kipande cha sanda na juu yake atafunikwa na madongo.

Hadithii hii ya mshumaa wa Sir Bobby Chalton kuzima jangwani imeufanya mji wa Manchester kupata simanzi kwasababu binadamu bora ameondoka mbele ya mboni za macho ya uso wa Dunia ya soka,Binadamu ambaye muda umechagua jina lake liandikwe Kwa wino wa dhahabu kwenye kitabu cha wafu na huzuni iwe zawadi njema pale kwenye nyasi za uwanja wa Old Traford.

Sir Bobby Charlton pumzika kwa amani tutaonana siku Balagumu litakapopulizwa kwa ajili ya binadamu kuhesabiwa haki,siku ambayo mbingu itafunguka, siku ambayo jua litawaka kwa hasira na mwezi kutembea kwa huzuni na wale watenda mema na dhambi watafufuliwa kutoka kwenye makuburini kwa ajili ya malipo huku macho na moyo vikiwa katika hali ya upofu.

Sir Bobby Charton juu ya kaburi lako sisi mashabiki wa Manchester United tutaweka Ile medali ya kombe la Dunia ulioshinda mwaka 1966, Medali tatu za ligu kuu na Ile ya kombe la Fa kuashiria Mwenyezi Mungu hakukosea kukupa zawadi ya uhai na kifo kwasababu umeutendea haki muda miaka 86 ulioishi chini ya Dunia iliyojaa chuki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live