Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rodrygo asema alidhalilishwa kwa ubaguzi wa rangi

Rodrygo Asema Alidhalilishwa Kwa Ubaguzi Wa Rangi Rodrygo asema alidhalilishwa kwa ubaguzi wa rangi

Fri, 24 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Mshambulizi wa Brazil Rodrygo amesema alidhalilishwa kwa ubaguzi wa rangi kwenye mitandao ya kijamii kufuatia mabishano makali na mchezaji wa Argentina Lionel Messi.

Wawili hao walirushiana maneno uwanjani huku mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia kati ya pande hizo mbili mjini Rio de Janeiro ikicheleweshwa kwa dakika 30 kwa sababu ya makabiliano makali kati ya polisi na mashabiki waliowatembelea.

Rodyrgo alisema alipokea jumbe zenye emoji za nyani na ndizi.

"Mitandao yangu ya kijamii ilivamiwa na matusi," Rodrygo aliandika kwenye Instagram.

"Tusipofanya wanavyotaka, tusipofanya wanavyofikiri, tukivaa kitu kinachowaudhi, tusipoinamisha vichwa vyetu wanapotushambulia, tukichukua nafasi wanafikiri ni wao peke yao, wabaguzi wataigiza tabia zao za uhalifu.

"Wabaguzi wa rangi daima wako kazini. Bahati mbaya kwao. Hatutakoma."

Messi alionekana akitangamana na nahodha wa Brazil Marquinhos na Rodrygo kabla ya wachezaji kadhaa wa Argentina kujaribu kutuliza hali iliyokuwa ikiendelea katika uwanja wa Maracana.

Baada ya kuchelewa kwa muda mrefu, mechi ya kufuzu Kombe la Dunia iliendelea, na Argentina ikashinda 1-0.

Chanzo: Bbc