Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rodrygo afichua kejeli za ubaguzi wa rangi anazofanyiwa

Messi Ms Rodrygo afichua kejeli za ubaguzi wa rangi anazofanyiwa

Fri, 24 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa Brazil na Klabu ya Real Madrid, Rodrygo Katika chapisho lake kwenye akaunti yake ya X (zamani ikijulikana kama Twitter), Rodrygo amefichua kuwa amekuwa akipokea matusi na kejeli za kibaguzi katika siku za hivi karibuni. Hii inakuja baada ya kuichezea Brazil huku wakipokea kichapo dhidi ya Colombia na Argentina .

"Wabaguzi wa rangi daima wanafanya kazi. Mitandao yangu ya kijamii imevamiwa na matusi na upuuzi wa kila aina.

Kama hatufanyi wanavyotaka, tusipofanya wanavyofikiri, tukivaa kitu kinachowasumbua na kuwakera ,tusipoinamisha vichwa vyetu tunaposhambuliwa, tukichukua nafasi wanazozipata.Wabaguzi watachukua hatua na tabia zao za uhalifu.

Lakini ni bahati mbaya kwao kwani hatutaacha!" - Rodrygo

Inasikitisha kuona kuwa kumekuwa na ongezeko la unyanyasaji wa kibaguzi unaowalenga wanasoka hasa kwenye mitandao ya kijamii. Vinicius Junior amewahi kufanyiwa hivyo ndani ya viwanja wakati akiichezea Real Madrid lakini kwa bahati mbaya sio nyota pekee ambaye amefanyiwa ubaguzi wa rangi hivyo tabia hii inapaswa kukemewa vikali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live