Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rodri amtupa mbalo Haaland Tuzo ya Ballon D'or

Rodri Ere Rodri

Wed, 21 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ndo hivyo. Supastaa wa Manchester City, straika la mabao, Erling Haaland huenda akaangukia kwenye nafasi ya tatu kwenye mchakato wa kusaka tuzo ya Ballon d'Or licha ya kuwa na takwimu tamu kabisa za msimu wa 2022-23.

Haaland aliongoza safu ya ushambuliaji ya Man City na kufanikiwa kunyakua mataji matatu makubwa ya msimu wa 2022-23, akiwa kinara wa mabao wa Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya pia.

Chama la Haaland, Man City lilinyakua ubingwa wa Ligi Kuu England, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la FA, ambapo waliwachapa mahasimu wao Manchester United katika mchezo wa fainali uliopigwa uwanjani Wembley.

Kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Man City waliichapa Inter Milan katika mchezo wa fainali uliofanyika huko Istanbul, Uturuki.

Mafanikio ya timu yake na ya kwake binafsi yalimfanya Haaland kuwa kwenye nafasi kubwa ya kuwania tuzo ya Ballon d’Or kwa mwaka huu.

Hata hivyo, mashabiki wa soka wanaamini kuna mchezaji mwenzake Haaland huko kwenye kikosi cha Man City, ndiye anayestahili tuzo ya Ballon d'Or na si mtambo huo wa mabao wa kocha Pep Guardiola.

Na mchezaji huyo si mwingine, bali ni Rodri, ambaye Jumapili iliyopita, aliongezea medali ya ubingwa wa Uefa Nations League kwenye kabati lake baada ya timu yake ya taifa ya Hispania kuichapa Croatia kwa penalti.

Kiungo, Rodri alisaidia La Roja kuichapa Croatia kwa penalti baada ya sare ya bila kufungana katika fainali iliyofanyika uwanjani De Kuip huko Rotterdam, Uholanzi.

Rodri, 26, alikuwa bora kwelikweli uwanjani, akipiga mzigo wa maana ule wa mchezaji bora wa mechi, akiendeleza tu moto wake kutoka kufunga kwenye fainali nyingine, wakati bao lake pekee lilipotosha kuwalaza Inter Milan kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuipa Man City ubingwa wao wa kwanza wa michuano hiyo mikubwa kabisa kwa ngazi za klabu.

Na kutokana na hilo, Rodri ambaye kwa mwaka huu ameshinda taji la Ligi Kuu England, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na klabu yake ya Man City na kisha kubeba Uefa Nations League akiwa na timu yake ya taifa ya Hispania, anajiweka kwenye nafasi kubwa ya kupigiwa kura ya kuwa mshindi wa Ballon d'Or 2023.

Straika wa kimataifa wa Norway, Haaland awali alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kushinda Ballon d’Or, huku supastaa Lionel Messi naye akijiweka pazuri kwenye kuongeza tuzo yake ya nane baada ya kuiongoza Argentina kunyakua Kombe la Dunia huko Qatar.

Lakini, Rodri mafanikio yake yanaweza kumsukuma Haaland hadi kwenye nafasi ya tatu kutokana na mashabiki kuamini wenzake wana nguvu zaidi.

Shabiki mmoja aliandika kwenye Twitter: "Ligi Kuu England, Kombe la FA, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Nations League. Mchezaji bora wa mechi kwenye fainali mbili. Rodri ameimaliza soka msimu huu."

Mwingine aliongeza: "Mkali wao wa msimu huu kiungo mkabaji Rodri anastahili kupanda pale kwenye kisemeo cha Ballon d’Or."

Shabiki wa tatu aliandika: "Kama Jorginho alikuwamo kwenye tatu bora ya Ballon D’or 2021, basi Rodri anapaswa kuwa mshindi wa Ballon D’or kwa kushinda mataji matatu na Nations League…mjadala unaosumbua."

Kuna shabiki ameandika: "Rodri ni mshindani halisi wa Ballon D'or kumzidi Messi."

Huku mwingine akiandika: "Umekuwa msimu mzuri sana wa 2022/2023 kwa Rodri. Tuzo ya Ballon d’Or ndiyo anayostahili."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live