Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robo tatu ya wachezaji wa Simba ni wagonjwa

Simba Pic Kikosi cha Simba chakabiliwa na magonjwa

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea mchezo wa NBC Tanzania, Simba dhidi ya Kagera Sukari Jumamosi ya kesho Desemba 18, 2021 mkoani Kagera, Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola amesema kikosi chake kinaandamwa na majeruhi.

"Tumekuwa na changamoto kidogo, Baadhi ya wachezaji nafikiri karibu robo tatu wamekuwa wakiumwa mafua, kifua na homa za hapa na hapa sijui inatokana na hali ya hewa au na nini, lakini na baadhi ya watu wa benchi la ufundi.

Kwahiyo nafikiri ndiyo changamoto tuliyonayo hadi sasahivi. Kwahiyo tumeacha madaktari wakiwa wanafanyakazi na kuweza kujua baadae itakuwaje kwa ajili ya mechi ya kesho, lakini mpaka sasahivi tuna changamoto ya wachezaji kuumwa," amesema Matola.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live