Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robo fainali zilizoacha gumzo Kombe la Dunia

E52B8591 90F3 4858 8DE2 99FBF55987A5.jpeg Aliyekuwa golikipa wa England, David Seaman

Sun, 11 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Fainali za Kombe la Dunia zimeshuhudiwa mechi za kibabe kabisa za hatua ya mtoano zilizowahi kutokea kwenye mchakamchaka huo wa kusaka ubingwa wa dunia.

Na hakika, hatua ya mtoano mara nyingi imekuwa na matukio ya kushtua na wakati mwingine hadi washindi wanapatikana kwa mikwaju ya penalti ili tu kupata fursa ya kunyakua taji hilo linalofahamika kwa jina la Jules Rimet.

Wakati hatua ya robo fainali ikitarajiwa kuanza leo Ijumaa huko Qatar, hizi hapa mechi za nane bora zilizowahi kuwa matata kabisa kwenye fainali zilizopita za Kombe la Dunia.

Uruguay 1-1 Ghana (2010)

Mechi hii ilikutanisha timu ya Amerika Kusini na Afrika na hakika imebaki kwenye kumbukumbu za kudumu kwa mashabiki kutokana na kile alichofanya Luis Suarez kudaka mpira makusudi ili kuwazuia Ghana wasifunge bao la ushindi kwenye dakika za mwisho.

Katika mchezo huo, Sulley Muntari aliifungia Black Stars bao la kuongoza, lakini halikudumu muda mrefu, Diego Forlan alisawazisha na kufanya ubao wa matokeo kusomeka 1-1. Baada ya dakika 90, ziliongezwa dakika 30 na hapo ndipo Suarez alipofanya tukio lake ambalo limebaki kumbukumbu hadi sasa. Kitendo cha Suarez kunawa mpira makusudi kulimfanya refa awape penalti Ghana na Asamoah Gyan akakosa mkwaju huo.

Dakika 120 zilifika tamati na matokeo yalibaki 1-1 kabla ya Uruguay kutinga hatua ya nusu fainali kwa mikwaju ya penalti, lakini Ghana wakibaki na hasira za Suarez kuwanyima fursa ya kufunga bao muhimu.

England 1-2 Brazil (2002)

Ronaldinho alikamatia shoo hiyo ya mwaka 2002 ambapo alifunga bao maridadi kabisa kwa upande wa Brazil na kuwatoa nje ya michuano England katika fainali zilizofanyika Japan na Korea Kusini. Katika mechi hiyo, England iliingia uwanjani kucheza na Brazil, ambayo ilikuwa haijabeba ubingwa kwa miaka minane. Na ikiwa na mastaa wengi wanaotamba kwenye Ligi Kuu England, Three Lions ilijiamini na kupata bao la kuongoza kupitia kwa Michael Owen.

Hata hivyo, bao hilo halikudumu sana, Rivaldo alisawazishia Brazil kabla ya Ronaldinho kumfunga kwa frii-kiki ya kushangaza kabisa kutoka umbali wa mita 40 akimtesa kipa David Seaman. Ronaldinho alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Danny Mills, lakini Brazil walilinda ushindi wao na kutinga hatua ya nusu fainali na ndio waliobeba ubingwa.

Uholanzi 2-1Argentina (1998)

Mechi baina ya Uholanzi na Argentina kwenye Kombe la Dunia 1998 ilikuwa na matukuo mengi, kadi za kutosha pamoja na mabao ya kutosha. Patrick Kluivert aliifungia Uholanzi bao la kuongoza kwenye dakika ya 12 tu ya mchezo, lakini Claudio Lopez akaisawazishia Argentina dakika tano baadaye. Katika dakika za mwisho, Arthur Numan alitolewa kwa kadi nyekundu katika dakika 15 za mwisho kabla ya Ariel Ortega kumpiga kichwa kipa Edwin van der Sar naye kutolewa nje. Na mechi hiyo ilimalizika kwa Oranje kufunga bao la pili kupitia kwa Dennis Bergkamp katika dakika za mwisho na hivyo kuwatoa Argentina na wao kutinga nusu fainali.

Argentina 2-1 England (1986)

Mechi ya kibabe kabisa, kwenye robo fainali ya Kombe la Dunia 1986, baina ya Argentina na England na siku zote itabaki kwenye kumbukumbu za kudumu. Staa, Diego Maradona alifunga bao lake la Mkono wa Mungu na kuwa gumzo duniani, huku akiwamaliza England katika fainali hizo zilizofanyika Mexico.

Maradona aliruka kichwa, lakini aliugusa mpira kwa mkono na bao hilo lilikubalika. Gary Lineker aliifungia bao England, lakini halikusaidia kitu, Argentina ilisonga mbele na kwenda kunyakua ubingwa huo kwa kuichapa Ujerumani Magharibi kwenye mchezo wa fainali.

Ureno 5-3 Korea Kusini (1966)

Ingawa mwaka 1966 unafahamika zaidi kwa England kushinda ubingwa wa dunia, lakini mechi iliyokuwa na mvuto zaidi ni ile ya robo fainali kati ya Ureno na Korea Kaskazini. Mechi hiyo ilishuhudiwa Ureno wakiwa nyuma kwa mabao 3-0 uwanjani Goodison Park na ilionekana kama watatupwa nje kabla ya Eusebio kupindua meza. Alifunga mabao manne Ureno ikashinda mechi hiyo kibabe mabao 5-3.

Chanzo: Mwanaspoti