Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robinho atupwa jela miaka tisa

Robinhos Robinho atupwa jela miaka tisa

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil, Robinho (40) ameambiwa na majaji nchini Brazil kwamba lazima atumikie kifungo cha miaka tisa jela kwa kosa la ubakaji nchini Italia.

Mwaka 2017, Robinho alihukumiwa nchini Italia kifungo cha miaka tisa jela kwa kitendo cha kushiriki katika kundi la unyanyasaji wa kingono ambalo walifanya kosa hilo mwaka 2013 kwenye Club moja ya usiku alipokuwa akiichezea AC Milan.

Kutokana na changamoto ya Taifa la Brazil kushindwa kukabidhi raia wake kwa nchi nyingine, ilipelekea Italia kutafuta kifungo chake katika taifa lake.

Mahakama ya Brazil sasa imeamua kwamba ni lazima atumike kifungo cha jela nchini Brazil na tayari majaji wa Mahakama ya Juu ya Haki ya nchini humo wamepiga kura kuthibitisha hukumu hiyo.

Kwa mujibu wa wakili wake, Robinho anataka kesi yake isikilizwe upya nchini Brazil kwa misingi ya uhuru wa kitaifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live