Sat, 18 Feb 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mahakama ya Milan nchini Italia inasisitiza kuwa Robinho arejee katika nchi hiyo kutumikia kifungo chake cha miaka 9 kwa kosa la ubakaji, hata hivyo, Robinho amekataa kuondoka Brazil.
Robinho na rafiki yake Ricardo Falcao walitiwa hatiani kwa kushiriki katika kitendo cha ubakaji nchini Italia mwaka 2013, na wawili hao walipatikana na hatia ya kufanya hivyo mwaka 2017.
Kulingana na Sheria za Brazil za kuwalinda raia wake, wawili hao hawataruhusiwa kwenda Italia.
Robinho na Falcao wana hatari ya kukamatwa ikiwa watasafiri nje ya Brazil.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live