Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robinho aanza kutumikia kifungo Brazil

Robinho Kifungo Robinho

Sun, 24 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Nyota wa zamani wa soka, Robinho, ameanza kutumikia adhabu ya kifungo cha miaka tisa jela baada ya mahakama ya Brazil kujiridhisha kuwa mshambuliaji huyo anapaswa kufanya hivyo akiwa kwao na sio Italia ambako alifanya makosa yaliyopelekewa apewe adhabu hiyo kali.

Robinho ambaye mwaka 2017 alikutwa na hatia ya ubakaji ambao alioufanya mwaka 2013 kwa mwanamke raia wa Albania akiwa na wanaume wengine watano, alifungua shauri la kutotaka kutumikia adhabu hiyo ya kifungo cha miaka tisa akiwa Brazil lakini hata hivyo imegonga mwamba.

Baada ya kumkuta na hatia hizo mwaka 2017, mahakama za Italia ziliamua kuziandikia zile za Brazil zikizitaka kutekeleza kwa adhabu hiyo kwa vile Robinho alitoroka nchini mwao na hakukuwa na uwezekano wa kumpata ili atumikie adhabu yake akiwa Italia.

Kutokanan na katiba ya Brazil kutotoa majibu ya moja kwa moja kama inawezekana au haiwezekani kwa Robinho kutumikia adhabu hiyo, jopo la majaji 15 lililazimika kupiga kura ambapo tisa kati yao waliamua kuwa Robinho aende jela huku wengine sita wakiamua tofauti.

Jopo hilo la majaji liliona kuwa kungetengenezwa mazingira rahisi kwa Robinho kutoroka nchini humo na hivyo suluhisho pekee kwake ni kutumikia adhabu hiyo, jambo ambalo limekuwa kama mkuki wa sumu kwa nyota huyo wa zamani wa Manchester City na Real Madrid.

Robinho alifanya kosa hilo la ubakaji wakati huo akiichezea AC Milan ambapo alikuwa na umri wa miaka 28, ingawa mwenyewe amedai kuwa kulikuwa na maelewani kati yake na mwanamke huyo aliyefanyiwa vitendo hicyo vya unyanyasaji wa kingono na ubakaji.

Mshambuliaji huyo anakumbukwa kwa kuichezea timu ya taifa ya Brazil katika mechi 100, akiifungia mabao 28 huku akipiga pasi za mwisho 23 na alionyeshwa kadi nane za njano.

Katika ngazi ya klabu, Robinho alicheza idadi kubwa ya mechi katika timu ya AC Milan ambayo aliitumikia katika mechi 144, akifunga mabao 32 na kupiga pasi 30 zilizozaa mabao.

Timu ambayo ililiweka kwenye chati jina la Robinho ni Real Madrid ambayo ilimnunua kutoka Santos mwaka 2005 kwa dau la Euro 24 milioni ambapo aliifungia mabao 35 na pasi 27 za mwisho katika idadi ya mechi 137.

Chanzo: Mwanaspoti