Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho ni Kibu na Malone tu Simba SC

Robertinho Kambini Uturuki.jpeg Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’

Wed, 9 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliviera Robertinho amemwagia sifa beki wake mpya, Che Fondoh Malone (24) raia wa Cameroon kwa kiwango alichokionyesha katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Power Dynamos kwenye kilele cha Simba Day.

Malone ambaye amejiunga na Simba akitokea Cotton Sports FC ya nchini kwao Cameroon, alianza kwa kucheza sambamba na Henock Inonga Baka kabla ya kipindi cha pili kucheza na Hussein Kazi aliyeingia naye dirisha hili la usajili akitokea Geita Gold.

Mara baada ya mchezo huo, Robertinho alionyesha kufurahia kiwango cha beki huyo pamoja na wachezaji wengine wapya huku akiamini wanaweza kuonyesha makubwa zaidi msimu huu wa 2023/24 kulingana na ambavyo wataendelea kuzoeana na wenzao.

“Nilitaka kuona vile ambavyo anaweza kucheza na wachezaji tofauti ndio maana tuliamua kumpumzisha Inonga, ni beki mzuri ambaye anaendana na staili yangu ya kutaka tushambulie kuanzia nyuma,”

Ikumbukwe pia Robertinho wakati akiwasili ndani ya Kikosi cha Simba Disemba mwaka Jana alionekana kuvutwa na Kibu Denis ambae alikuwa akitazamwa vibaya na Wanasimba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live