Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho mambo magumu Simba, apewa mechi tatu

Baleke Robertinho E Robertinho na Kanoute

Wed, 22 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imeelezwa kuwa hatma ya Kocha Mkuu wa Simba, Mbrazil Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ipo katika michezo miwili ya hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na mmoja wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Simba ina malengo mawili katika msimu huu ambayo ni kubeba kombe la ligi na FA sambamba na kufuzu hatua ya robo fainali kimataifa.

Timu hiyo, katika Kundi lao, C ipo mkiani wakiwa hawana pointi ambapo wamepoteza mechi mbili za kwanza walizocheza, walianza kwa kufunga bao 1-0 na Horoya kabla ya kuchapwa 3-0 na Raja Casablanca.

Taarifa ambazo Tanzaniawebimepenyezewa ni kwamba, kocha huyo amepewa michezo hiyo mitatu watakayoicheza Simba wa kwanza ni wa ligi dhidi ya Azam FC jana Jumanne saa moja usiku kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa mchezo huo dhidi ya Azam ni muhimu kwao kupata ushindi, kwani ndio utaamua hatima ya ubingwa wa ligi ambao unatetewa na Yanga.

Aliongeza kuwa mingine miwili ya kimataifa dhidi ya Vipers SC ya Uganda ambao Simba watakuwa wageni utakaochezwa nchini Uganda kabla ya kurudiana na timu hiyo, nyumbani kwenye Uwanja wa Mkapa.

“Simba wanataka heshima katika msimu huu, hivyo Bodi ya Wakurugenzi wa timu hiyo, walimuwekea malengo katika mkataba wake kabla ya kuusaini.

“Ambayo ni kuchukua ubingwa wa ligi na mchezo wetu dhidi ya Azam ndio utakaoamua hatima yetu, ni lazima tupate ushindi ili tuendelee tuwepo katioka vita dhidi ya wapinzani wetu Yanga.

“Mingine hii miwili inayofutia ya mfululizo dhidi ya Vipers tutakaoanzia ugenini na nyumbani ambayo lazima yote tushinde ili tujiweke katika nafasi nzuri ya kufuzu ribo fainali kimataifa, hivyo kocha ni lazima apambane na benchi la ufundi kuhakikisha tunashinda michezo yote hiyo ili ajiweke salama,” alisema mtoa taarifa huyo.

Kocha huyo juzi alizungumzia matokeo mabaya waliyoyapata dhidi ya Horoya AC na Raja Casablanca na kusema kuwa “Nimejipanga kupata matokeo mazuri ya ushindi dhidi ya Vipers tutakapocheza ugenini kabla ya kurudiana nyumbani.

“Lakini ninahitaji muda zaidi wa kuijenga timu imara na kutumia, kwani tangu nimejiunga na Simba kupata muda mwingi wa kuandaa timu na badala yake kucheza michezo ya mfululizo bila kupumzika,” alisema Robertinho.

KUNDI LA SIMBA CAF

P    W D   L    GF GA Pts

1.Raja CA      2    2    0    0    8    0    6

2.Horoya       2    1    1    0    1    0    4

3.Vipers         2    0    1    1    0    5    1

4.Simba         2    0    0    2    0    4    0

Chanzo: www.tanzaniaweb.live