Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho kwenye presha kubwa Simba

Roberto Robertinho.jpeg Robertinho kwenye presha kubwa

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya kufanikiwa kuivusha Simba hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira yuko katika presha kubwa

Baada ya mchezo dhidi ya Power Dynamos uliopigwa uwanja wa Azam Complex jana na Simba kulazimishwa sare ya bao 1-1 matokeo ambayo yalitosha kuwapeleka Wekundu wa Msimbazi makundi kwa faida ya mabao mawili waliyofunga ugenini, bodi ya Wakurugenzi ya Simba ilikutana kwa dharura kujadili kile kilichoelezwa kutoridhishwa na kiwango cha timu.

Msimu huu mashabiki wa Simba wametoa malalamiko karibu kila baada ya mechi kutoridhishwa na kiwango cha timu yao licha ya kupata matokeo mazuri.         Hofu iliyopo ni kwamba hakuna uhakika kama Simba itaweza kufikia malengo yake ya kushinda nataji yote ya ndani pamoja na kucheza nusu fainali ya ligi ya mabingwa kama timu itaendelea kucheza kama ilivyo sasa.

Miongoni mwa waliotoa malalamiko ni Rais wa heshima wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji ambaye kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii aliandika ujumbe unaoashiria haridhishwi na kile alichokishuhudia.

Katika misimu iliyopita, Simba ilidumisha utamaduni wake wa kucheza kandanda safi iliyoambatana na ushindi na zaidi kwenye michuano ya Kimataifa Simba imejijengea heshima ya kuwa timu hatari sana inapocheza mbele na mashabiki wake Robertinho amekuja na falsafa tofauti ambapo jambo muhimu kwake ni timu kupata matokeo mazuri pasipo kujali wamecheza vipi.

Mpaka sasa Robertinho amefanikiwa katika mbinu zake, hajapoteza mchezo katika mechi tisa zilizopita.

Mwanzoni mwa msimu huu aliiongoza Simba kutwaa Ngao ya Jamii na ameweza kushinda mechi zote tatu katika ligi kuu pamoja na kuipeleka Simba hatua ya makundi CAFCL.

Hata hivyo presha ya mashabiki ambao hawaridhishwi na vile timu yao inacheza, imepata nguvu zaidi baada ya kuanza kuungwa mkono na baadhi ya viongozi Pengine Robertinho na benchi lake la ufundi wanapaswa kufanya kitu haraka kwa kuanzia mechi inayofuata kwenye ligi kuu dhidi ya Prisons itakayopigwa Alhamisi huko Mbeya.

Baada ya mechi hiyo Simba inakabiliwa na mechi mbili za AFL dhidi ya Al Ahly, mchezo wa kwanza ukipigwa Oktoba 22 uwanja wa Benjamin Mkapa na marudiano kupigwa Oktoba 24 huko Misri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live