Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho kufanya mabadiliko ya kikosi dhidi ya Al Ahly

Robertinho Kufanya Mabadiliko Ya Kikosi Dhidi Ya Al Ahly Robertinho kufanya mabadiliko ya kikosi dhidi ya Al Ahly

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema anafahamu mchezo wa kesho dhidi ya Al Ahly utakuwa mgumu hivyo kuna mabadiliko atayafanya kwenye kikosi.

Robertinho ametoa kauli hiyo leo Oktoba 23, 2023 alipokuwa akizungumzia mchezo huo war obo fainali ya pili ya African Football League baada ya ule wa awali kupata sare ya 2-2 jijini Dar.

“Nafahamu tutakuwa na mechi ngumu kesho dhidi ya timu kubwa Afrika ila kuna namna ambavyo tutaingia na mpango tofauti na ilivyokuwa kwenye mchezo wa kwanza nyumbani. Nitakuwa na mabadiliko ya wachezaji kwenye baadhi ya maeneo ili kufanikiwa kucheza vizuri na kupata ushindi,” alisema Robertinho. Mechi hiyo itapigwa keshi nchini Misri majira ya saa 11:00 jioni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live