Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho hana presha kumkosa Chama kesho

Chama Best Goal Robertinho hana presha kumkosa Chama kesho

Wed, 9 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Simba Clatous Chama anatarajiwa kukosa mchezo wa nusu fainali wa Ngao ya Jamii dhidi ya Singida FG.

Mchezo huo utapigwa kesho Alhamisi, Agosti 10, 2023 katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Chama anatumikia adhabu ya kukosa mechi tatu baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting msimu uliopita.

Chama alikosa mechi dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union katika msimu uliopita na mechi ya nusu fainali dhidi ya Singida FG itakuwa ya mwisho

Licha ya kumkosa Chama, kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira hatakuwa na hofu yoyote kwani ana kikosi kipana chenye wachezaji bora zaidi ya mmoja katika kila nafasi.

Luis Miquissone, Aubin Kramo, Willy Onana wote wanaweza kutumika katika nafasi ambayo hucheza Chama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live