Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho awatetea nyota wake kushinda wakiwa na uchovu

Robertinho X Jose Luis Miquissone Robertinho awatetea nyota wake kushinda wakiwa na uchovu

Sun, 8 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera 'Robertinho' amewatetea wachezaji wake kwa kushinda mchezo dhidi ya Singida FG wakiwa na uchovu wa safari na mechi mfululizo.

Robertinho ametoa kauli hiyo leo Oktoba 8, 2023 mara baada ya kuifunga Singida 2-0 katima dimba la CCM Liti mkoani Singida.

"Kipindi cha kwanza tumecheza vizuri na lazima niwapongeze wachezaji wangu wametoka kucheza mechi mfululizo, uchovu wa safari lakini tumepata alama tatu," alisema Robertinho.

Kwa ushindi huo, Simba wamekwea kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC kwa kufikisha alama 15, wakifuatiwa na Azam FC wenye alama 13 huku wapinzani wao Yanga wakiwa nafasi ya tatu na alama zao 12.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live