Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho awatangazajia 'kiama' Ihefu FC

Robertinho Kufanya Mabadiliko Ya Kikosi Dhidi Ya Al Ahly Robertinho awatangazajia 'kiama' Ihefu FC

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera 'Robertinho' amesema amrejea kwenye mapambano ya Ligi Kuu ya NBC na kwamba hakuna namna, lazima awatandike Ihefu FC hapo kesho Oktoba 28, 2023.

Robertinho ametoa kauli hiyo kueleka mchezo wao huo wa raundi ya saba unaotarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

"Tumerejea kwenye ligi baada ya kumaliza michuano ya African Footbal League, jana nilipata nafasi ya kuwatazama wapinzani wetu Ihefu, wana timu nzuri lakini sisi tupo kwenye hali nzuri kwa sasa na tumejipanga kupata ushindi," alisema Robertinho.

Robertinho ametolewa kwenye mashindano ya AFL hatua ya Robo Fainali baada ya kupata sare ya 2-2 nyumbani na kisha sare ya ugenini ya 1-1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live