Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho awapongeza Yanga, aukubali mziki wao

Robertinho Yangaaaa Robertinho awapongeza Yanga, aukubali mziki wao

Mon, 6 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera 'Robertinho' amewapongeza wapinzani wao wa jadi Yanga SC kwa kushinda dabi waliyoipiga jana Novemba 5, 2023 na kuibuka na ushindi wa 5-1.

Akizungumzia mchezo huo mara baada ya kumalizika kwa Simba kupoteza kwa kichapo hicho kizito, Robertinho amesema, wachezaji wake kipindi cha kwanza walicheza vizuri lakini kipindi cha pili walikuwa wanaacha nafasi kubwa kwa mpinzani.

"Walikaa nyuma sana na kutoa nafasi kwa mpinzani kufunga magoli mawili haraka lakini kimsingi niwaponmgeze wapinzani, wamecheza vizuri kipindi cha pili na kushinda dabi," alisema Robertinho.

Yanga wamezidi kujikita kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha alama 21 wakiwa wamecheza michezo nane huku Simba akishika nafasi ya tatu akibaki na alama zake 18 kwa michezo yake saba aliyocheza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live