Wakati Simba ikijiandaa na michezo yake miwili muhimu wa kwanza ukiwa ni ule wa Kombe la Shirikiso la Azam Sports hatua ya 16 bora dhidi ya Klabu ya African Sports Machi 2.
Kocha Mkuu wa Kikosi cha Simba Mbrazil Roberto Oliveira "Robertinho" amewataka Mashabiki wa Simba kujitokeza Uwanjani kuwapa sapoti;
Akizungumza Robertinho amesema;
"Tumejipanga kuhakikisha tunashinda mchezo wa kesho wa ASFC dhidi ya African Sports. Tunategemea kuwatumia Wachezaji ambao hawajapata nafasi kubwa kikosini kwa kuwa tuna mchezo wa marudiano nyumbani dhidi ya Vipers kwa hiyo tunaziangalia mechi zote."
Mchezo huo utapigwa katika Uwanja wa Uhuru kuanzia majira ya saa 10:00