Kocha Mkuu wa timu ya Simba SC, Roberto Oliveira 'Robertinho', ameondoka nchini Uturuki ambapo timu hiyo, ipo kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao, na kuelekea nchini Brazil, kwa ajili kuhudhuria kozi fupi ya masomo ya ukocha (FIFA Pro License) yanayofanyika Brazil.
Taarifa hiyo imetolewa na timu hiyo ambapo imebainisha kuwa Robertinho atakuwa Brazil kwa muda wa wiki moja na atarejea Uturuki Julai 24, 2023, baada ya mafunzo hayo kumalizika.
Ikumbukwe kuwa, Simba imeondoka wiki hii kwenda nchini Uturuki kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi kuelekea msimu mpya wa 2023/24 ampapo kambi hiyo itafanyika kwa wiki tatu kabla ya kurejea nchini.
Baadhi ya nyota wake bado hawajaondoka kwenda Uturuki kuungana na wenzao, ambapo waliobaki ni Clatous Chama, Jean Baleke, Fabrice Ngoma, Che Fondoh Malone, Pape Sakho, Kramo Kouame na Willy Onana ambao wanatarajia kuondoka nchini Julai 17 2023.