Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho atenga dakika 120 za maangamizi

Robertinho Mkwara Kocha Robertinho

Sat, 3 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kikosi chake kurejea kambini juzi Alhamisi, Kocha Mkuu wa Simba, Mbrazil Roberto Olivieira ameweka wazi kuwa wameandaa programu ya mazoezi ya siku tano sawa na saa 120 kumaliza hesabu zao za msimu huu na kuanza rasmi maandalizi ya msimu ujao.

Simba wamesaliwa na michezo miwili ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Juni 6, mwaka huu kabla ya kumalizana na Coastal Union Juni 9, mwaka huu.

Kwenye msimamo, Simba wanakamata nafasi ya pili na pointi zao 67 walizokusanya kwenye michezo 28 waliyocheza, wakishinda mechi 20, sare saba na kupoteza mchezo mmoja.

Simba inaendelea na mazoezi hayo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Simba MO Arena chini ya kocha huyo maarufu  kama Robertinho pamoja na wasaidizi wake.

Akizungumza nasi, Robertinho alisema: “Jambo zuri kwetu ni kuwa kikosi kimerejea kambini kwa ajili ya kumalizia maandalizi yetu ya michezo miwili iliyosalia na tumeandaa programu ya siku tano kumaliza kabisa hesabu za msimu huu.

“Baada ya michezo dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union ambayo itakuwa mwisho rasmi wa msimu kwetu tunatarajia kutoa mapumziko ya muda kwa wachezaji wote kabla ya kurejea kwa ajili ya maandalizi ya kabla ya msimu ‘pre season’ ya msimu ujao.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live