Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho atangaza ujio wa Phiri, awatangazia kiama Namungo

Robertinho X Phiri Moses Phiri yuko fiti baada ya majeraha ya muda mrefu

Sun, 30 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha fundi wa mbinu, Robertinho amezungumzia kurejea kwa mshambuliaji na kinara wa mabao katika Ligi Kuu katika timu hiyo, Moses Phiri aliyefunga 10.

“Phiri ni mchezaji mzuri na hakuna asiyejua umuhimu wake lakini mashabiki zetu wanapaswa kutambua hakuweza kucheza sana kutokana na majeraha aliyokuwa nayo hivyo tulihitaji kumuona akiwa fiti kimwili na kiakili.”

Phiri alikosekana uwanjani tangu alipopata majeraha ya nyonga katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar uliopigwa Desemba 21, mwaka jana kwenye Uwanja wa Kaitaba akicheza rafu ya kihuni na kiungo Makame.

Mchezo ujao kwa Simba utakuwa ni ule wa Ligi Kuu dhidi ya Namungo FC utakaopigwa Mei 3 kwenye Uwanja wa Majaliwa mjini Ruangwa kisha kucheza na Azam FC Mei 6 katika Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) hatua ya nusu fainali itakayopigwa katika Uwanja wa Nang-Lwanda Sijaona, Mtwara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live