Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho atangaza mpango mpya kuikabili Yanga kesho

Robertinho 5.jpeg Robertinho atangaza mpango mpya kuikabili Yanga kesho

Sat, 4 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera 'Robertinho' ametangaza kuingia na mpango mpya katika mechi ya kesho dhidi ya mtani wake Yanga SC.

Robertinho ametoa kauli hiyo leo Novemba 4, 2023 alipokuwa akielezea maandalizi yake kuelekea dabi hiyo kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati.

"Tuna mpango mpya kwa ajili ya mchezo wa kesho kwa maana kila mechi inakuwa na mahitaji yake. Naamini kwenye viwango na uwezo wa wachezaji wangu na wale waliofanya vizuri kwenye mazoezi wiki hii nitawapatia nafasi ya kuanza kesho. Uzuri ndani ya kikosi changu kuna wachezaji wa michezo mikubwa ya aina hii," alisema Robertinho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live