Kocha mkuu wa Simba, Roberto Oliveira 'Robertinho' amesema maandalizi yamekamilika na sasa kikosi chake kinasubiri muda ufike wakatafute alama tatu dhidi ya Al Ahly kesho Oktoba 20 katika dimba la Mkapa saa 12:00 jioni.
Michuano ya African Football League (AFL) imelenga kukuza, kurithisha na kulipa thamani soka la Afrika ambapo katika msimu wake wa kwanza ambao unazinduliwa rasmi kesho itahusisha timu nane pekee, ambazo zimechaguliwa kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo ubora na umaarufu wa klabu lakini kwa msimu utakaofuata timu zitaongezeka na kuwa 22.
"Ni mechi ngumu kwetu lakini tumejiandaa kushinda, ni wa kati wetu kuionyesha dunia ukubwa tulionao na naamini kesho, kila mtu ataiona Simba ikishinda," alisema Robertinho ambaye wachezaji wake wote wapo kambini wakiingoja mechi hiyo.
Kwa upande wa kocha wa Ahly, Marcel Koller alisema anajua ugumu wa Simba na anaamini anakuja kucheza na timu inayokamia.
"Simba inatimu nzuri, najua watacheza kwa kukamia lakini tumejiandaa kuwakabili," alisema Koller